Loading...

KAKAYAKE MESSI AHUKUMIWA KWA KUPATIKANA BUNDUKI KINYUME NA SHERIA

Loading...
Kakayake mkubwa nyota wa Barcelona Lionel Messi, Matias amehukumiwa kwa kupatikana na bunduki kinyume na sheria.

Jamaa huyo mwenye miaka 36 lihukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela mnamo Alhamisi, Agosti 16, lakini badala ya kutumikia kifungo atafanya huduma kwa jamii.

Kulingana na ripoti kutoka kwa gazeti la Argentina La Capital, waendeshaji mashtaka walikutana kabla ya kufikia uamuzi wa matias kutoenda gerezani.

Aidha, ripoti hiyo ilisema bunduki hiyo ilipatikana mnamo 2017, dani ya meli iliyojaa damu ambapo Matias alianguka katika Mto Parana. 

Wakili wa Matias pia alisemekana kuhoji kwamba mteja wake alianguka katika meli hiyo na kukanusha kwamba alimiliki bunduki hiyo. 

Ndiye ndugu wa katikati wa familia ya Messi huku Rodrigo akiwa na miaka 38 naye ionel akiwa na miaka 31.

Watatu hao pia wana dada mdogo kwa jina Maria, ambaye ana miaka 31.

Wakati huo huo Messi anajiandaa kwa msimu mpya wa La Liga baada ya mapumziko ya kombe la Dunia FIFA WORLD CUP 2018.

Mabingwa wa Uhispania Barcelona mnamo Jumatano usiku Agosti 15, waliwashinda Boca Juniors 3-0 katika mechi yao ya awamu ya mwisho waliposhinda Tuzo la Joan Gamper Trophy.

Mchezaji mpya Malcom aliyejiunga kutoka Bordeaux msimu huu alifunga bao la kwanza katika dakika ya 18. 

Lionel Messi alifunga bao la pili katika dakika ya 39 kabla ya Rafinha kutia kimiani bao la tatu katika dakika ya 67.
Na Peter Godwin.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KAKAYAKE MESSI AHUKUMIWA KWA KUPATIKANA BUNDUKI KINYUME NA SHERIA KAKAYAKE MESSI AHUKUMIWA KWA KUPATIKANA BUNDUKI KINYUME NA SHERIA Reviewed by By News Reporter on 8/20/2018 11:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.