Loading...

PATA KUJUA MAKUNDI MAWILI YA BINADAMU KULINGANA NAMNA WANAVYOFIKIRI MAISHA YAO

Loading...
Tunaweza kuwatenga watu katika makundi  mawili kulingana na namna wanavyofikiri kuhusu maisha yao.

Kundi la kwanza linaundwa na wale watu ambao wao wanatumia muda wao kufikiri juu ya mambo ambayo hawayapendi yatokee katika maisha yao. Ukiwauliza wanatamani nini katika maisha yao moja kwa moja wanaanza kuorodhesha mambo ambayo hawapendi yatokee katika maisha yao.

Kundi la pili linaundwa na wale watu ambao wao hufikiri juu ya mambo ambayo wanayataka katika maisha yao. Wakiulizwa, wao moja kwa moja huanisha vitu/mambo wanayoyataka.

Ukitazama kwa haraka unaweza usibaini tofauti ya makundi haya. Aina hizi mbili za fikra zina matokeo tofauti, fikra za kundi la kwanza zimelenga kuepuka mambo fulani na fikra za kundi la pili zimejikita kutafuta kufanikisha mambo ambayo wanayataka.

Uko katika kundi gani? Muda wako mwingi unawaza nini? Unawaza juu ya aina ya maisha usiyoyataka au unawaza juu ya aina ya maisha unayoyataka. Ukijikita katika kufikiri kile unachokitaka unakuwa katika nafasi nzuri ya kufanikiwa na kupata kile unachokitaka.

Keep Moving Forward!
Vicent Stephen



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
PATA KUJUA MAKUNDI MAWILI YA BINADAMU KULINGANA NAMNA WANAVYOFIKIRI MAISHA YAO PATA KUJUA MAKUNDI MAWILI YA BINADAMU KULINGANA NAMNA WANAVYOFIKIRI MAISHA YAO Reviewed by By News Reporter on 8/20/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.