Loading...

KENYA YAZUIA UINGIZAJI WA VIGAE TOKA TANZANIA

Loading...
Nchi ya Kenya imezuia uingizwaji wa vigae  vinavyotoka Tanzania hali iliyosababisha kudorola kwa soko hilo nchini.

Hayo yalisemwa jana na Msafiri Figa Meneja Uajiri kutoka kiwanda kinachozalisha vigae cha Goodwill Tanzania Cerami co. Ltd kilichopo Mkiu, wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Alisema ,walikuwa wakitegemea soko la Kenya zaidi kutokana na kupata oda nyingi kutoka kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo .

Figa alisema ,kipindi kiwanda kinaanza lengo lao ilikuwa kuzalishaji mita za mraba 80,000  sawa na vigae 800,000 kwa siku lakini kwa sasa tangu waanze kuzalisha wanazalisha vigae 600,000 kwa siku .

Figa alielezea, wana wafanyakazi 900 kutoka Tanzania,ajira zisizo za moja kwa moja 2,000-3,000 na wachina 60 ambao ni pamoja na wataalamu mbalimbali..

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ,alisema hali iliyopo ni hatari kwani inakwenda kuuwa viwanda na kuweka hofu ya kuzima ndoto yetu.

“Mwaka mmoja na nusu uliopita eneo hili lilikuwa pori ambapo sasa kuna kiwanda kikubwa ambacho kinatengeneza ajira na kuliingizia mapato Taifa”

Ndikilo alieleza ,tatizo la ukosefu wa soko sio la kubeza ,sio la masihala,hivyo amekiomba chama kisimamie hilo.

Alisema ,wapo wafanyabiashara wanaagiza vigae China suala hili linakandamiza wawekezaji wa ndani .

“Wapo watendaji serikalini wanaotoa vibali kwa wanyabiashara kuagiza nondo Uturuki na vigae China,Spain na wengine kuchukua chuma nje hivyo kuna kila sababu kuliangalia tatizo hilo” alisisitiza Ndikilo.

Alisema, serikali inafanya kazi lakini baadhi ya watendaji wanasababisha tatizo hili kwa maslahi binafsi.

Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KENYA YAZUIA UINGIZAJI WA VIGAE TOKA TANZANIA KENYA YAZUIA UINGIZAJI WA VIGAE TOKA TANZANIA Reviewed by By News Reporter on 8/16/2018 07:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.