Loading...

SAVIMBI KUZIKWA KWA HESHIMA KABLA YA MWISHO WA MWAKA HUU

Loading...
Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa waasi Chief Jonas Savimbi, aliyeuawa mwaka 2002, utapatikana kabla mwisho wa mwaka ili uzikwe 'kwa heshima,' chama chake kilisema Jumatano.

Isaias Samakuva, kiongozi wa sasa wa chama cha National Union for the Total Independence of Angola (Unita) walitangaza kwa vyombo vya habari baada ya kikao na rais wa nchi, Joao Luurenco huko Luanda.

Alisema "amepata kibali" kutoka kwa Lourenco kwamba mabaki ya Savimbi "Yatapatikana kabla ya mwisho wa mwaka huu".

Savimbi ambaye alikuwa mtu katili, kaidi na gaidi aliyekuwa mkuu wa vita, ambaye alikuwa akiipiga serikali ya kijamaa ya Angola kwa muda wa miaka 27, aliuawa katika mapigano na jeshi la Angola mnamo Februari 22, 2002.

Kifo chake kiliperekea makubalino ya amani na kumaliza vita ya umwagaji damu iliyodumu kwa muda mrefu, ambayo ilizuka baada ya kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975.

Wiki sita baada ya kifo chake, chama chake cha kiharakati cha UNITA waliweka walitiasaini makubaliano ya amani na serikali.

Alizikwa siku iliyofuata katika jimbo la Mexico mashariki mwa Angola, ambapo alipofariki.

Samakuva mapema ya mwezi huu alishuku serikali kukataa maziko ya heshima ya savimbi ambapo alielezea kuwa ni unyanyapaaji.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
SAVIMBI KUZIKWA KWA HESHIMA KABLA YA MWISHO WA MWAKA HUU SAVIMBI KUZIKWA KWA HESHIMA KABLA YA MWISHO WA MWAKA HUU Reviewed by By News Reporter on 8/16/2018 07:11:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.