Loading...

VISA NA MIKASA: DUNIA IMEKWISHA, MAMA APACHIKWA MIMBA NA MWANAWE

Loading...
Mwanamke mmoja ameripotiwa kulala na mwanae ili kumpachika mimba nchini Nigeria.

Veronica Iorshe mwenye umri wa miaka 47 alilala na mwanae aliyemzaa na mumewe wa kwanza aliyefariki.

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliamua kufanya kitendo hicho baada ya familia ya mumewe kulalamila kuwa hakuwa na uwezo wa kuzaa. 

Veronika alikuwa ameishi na mumewe huyo wa pili kwa zaidi ya miaka minane bila kujaliwa mtoto, hii ni baada ya mumewe wa kwanza kufariki na kumuacha na mtoto mmoja.

Sebestian ambaye ni mumewe wa pili vile vile alifiwa mke wa kwanza kabla kujaliwa mtoto naye. 

Baada ya kuishi na veronica kwa miaka kadhaa, familia ya Sebastian ilianza kulalamika wakidai kuwa mwanao alimuoa mwanamke asiye na mbegu. 

Veronika alimsihi mumewe waende katika vipimo ili kubainisha yule ambaye ana shida lakini akadinda.

Hapo ndipo Veronika alimposhawishi mwanae mwenye umri wa miaka 26 kulala naye na moja kwa moja akampachika mimba. 

Aliporudi nyumbani na ujumbe huo mzuri kwa mumewe, jamaa huyo alimkataa na kutaka waende hospitalini kubaini kama kweli mtoto alikuwa wake.

Jaribio zilithibitisha kuwa jamaa huyo alikuwa na upungufu wa mbegu na hivyo hangeweza kumpachika mwanamke mimba. 

Mambo yalipozidi kuchacha, Veronika alilazimika kukiri kuwa alilala na mwanae aliyempachika mimba.
Na Catherine Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: DUNIA IMEKWISHA, MAMA APACHIKWA MIMBA NA MWANAWE VISA NA MIKASA: DUNIA IMEKWISHA, MAMA APACHIKWA MIMBA NA MWANAWE Reviewed by By News Reporter on 8/16/2018 06:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.