Loading...
Mashabiki wa kandanda walishuhudia kioja wakati wa droo za UEFA Champions League Moscow wakati mahasimu wa kandanda Mohammed Salah na Sergio Ramos walikutana ana kwa ana kwa muda mfupi.
Wawili hao walipamba vichwa vya habari Mei 28 mwaka huu, Salah alipoumizwa bega na mlinda mlango huyo wa Real Madrid.
Liverpool wakati huo ilipoteza 3-1, katika kisa ambacho Ramos alitupiwa lawama.
Ramos alijitetea sana kuhusu tetesi kwamba alimuumiza Mo Salah ambaye ana mashabiki wengi zaidi Anfield.
Walipokutana usiku wa droo za UEFA, Ramos alionekana kuendeleza hila zake, kama walivyofikiria baadhi ya mashabiki.
Ramos alimpokea mchezaji huyo wakati wa droo na alipokuwa akirejea kuketi, alimgota begani kwa upole kutokana na kuwa alikuwa ameketi mbele yake.
Hilo lilizua mjadla katika mitandao ya kijamii huku mashabiki wakitaniana kuhusu wachezaji hao na kisa hicho.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KIOJA ALICHOKIFANYA RAMOS BAADA YA KUKUTANA ANA KWA ANA NA MO SALAH
Reviewed by By News Reporter
on
8/31/2018 09:48:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: