Loading...

VISA NA MIKASA: JAMAA ATUPWA JELA MIAKA 2 KWA KUIBA MSWAKI

Loading...
Mahakama moja Kisumu - Kenya, ilimpa mwanamume kifungo cha miaka miwili na nusu gerezani baada ya kukubali kuiba bidhaa za nyumbani ikiwemo ni pamoja na mswaki na kalamu.

Felix Ouma alikubali kuiba bidhaa hizo kutoka nyumbani mwa Gervin Owino, katika mtaa wa mabanda wa Obunga, Kaunti ya Kisumu Agosti 6 na Agosti 23, 2018.

Katika ripoti iliyoandikwa na Standard, mshukiwa mwenzake Frank Onyango, alikana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya Tsh. 1.1 Milioni akingoja kusikilizwa kwa kesi dhidi yake.

Hakimu Mkuu Christopher Yalwala wa Mahakama ya Kisumu alimpata Ouma na makosa ya kuvunja nyumba ya mlalamishi na kuiba spika nne, simu, mtungi wa gesi, TV, curtain, kifaa cha kupuzilia hewa zote za thamani ya Tsh 803,750.

"Mlalamishi alikuwa ameondoka nyumbani kwake saa moja usiku kununua vitu na aliporudi alipata nyumba yake imevunjwa na vitu kuchukuliwa,” ilisema hati ya mahakama. Katika kisa kingine, wawili hao walishutumiwa kuiba mswaki, kitambaa, kalumu mbili, earphones, charger ya simu na vitu vingine vya thamani ya TSh 98,334.

Sufuria mbili pia zilipatikana na chifu wa eneo hilo na zilitolewa makamani kama ushahidi.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: JAMAA ATUPWA JELA MIAKA 2 KWA KUIBA MSWAKI VISA NA MIKASA: JAMAA ATUPWA JELA MIAKA 2 KWA KUIBA MSWAKI Reviewed by By News Reporter on 8/31/2018 10:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.