Loading...

YOUNG DEE MAJI YA SHINGO, ADAI YUKO TAYARI KWENDA MAHAKAMANI NA UONGOZI WAKE

Loading...
Rapa Young Dee a.k.a Pakarasta amesema hayupo sawa na uongozi wake wa #KingCAsh na kuamua kuanzisha kampuni yake iitwayo 'Dream City World Wide', huku akidai yupo tayari kuenda Mahakamani endapo meneja wake huyo atataka kufuata sheria zaidi juu yake. 

Young Dee ameeleza hayo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kuenea tetesi kuwa uongozi huo unampango wa kumfungulia mashtaki rapa huyo, kwa kile kinachodaiwa kuvunja mkataba waliowekeana kipindi walipokuwa pamoja wakifanya kazi. 

"Mimi nimefuata kila kitu kisheria na kuhusu mkataba kama anataka kufanya chochote afate sheria. Mimi nipo tayari hata kwenda Mahakamani", amesema Young Dee. 

Pamoja na hayo, Young Dee ameendelea kwa kusema "nilikuwa na malengo yangu ambayo nilijiwekea, ila nimegundua baada ya muda fulani kwamba mambo hayakuwa sawa 'so' kwasababu mimi ni mwanaume na nina majukumu yangu. Nimeamua ku-step up kama mwanaume katika kujisimamia kazi zangu mwenyewe". 

Rapa Young Dee ni miongoni mwa wasanii walioingia katika tasnia hiyo wakiwa na umri mdogo, na hadi hii leo bado yupo kwenye game anafanya vizuri.
Na Hamisi Fakhi.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
YOUNG DEE MAJI YA SHINGO, ADAI YUKO TAYARI KWENDA MAHAKAMANI NA UONGOZI WAKE YOUNG DEE MAJI YA SHINGO, ADAI YUKO TAYARI KWENDA MAHAKAMANI NA UONGOZI WAKE Reviewed by By News Reporter on 8/31/2018 12:10:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.