Loading...

BOBI WINE AKAMATWA TENA, AZUILIWA KWENDA KUTIBIWA NJE

Loading...
Saa chache baada ya kukamatwa kwa mbunge wa Kyadondo Mashariki Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine, katika uwanja wa ndege wa Entebe polisi wamempeleka katika hospitali ya Kirudu Uganda. 

Kulingana na mke wake Barbie Kyagulanyi, alipelekwa kwa nguvu hospitalini huku polisi wakiashiria walikuwa wakisubiri maagizo kutoka kwa idara husika kuhusu hatua itakayofuata.

Katika taarifa aliyochapishwa Facebook mnamo Alhamisi, Agosti 30, Barbie alipuuzilia mbali ripoti za awali kwamba mbunge huyo alikuwa ametoweka kutoka hospitali ya Lubaga ambapo alikuwa akipokea matibabu.

Pia alisema mbunge huyo alimtobolea siri kuwa aliteswa kwa mara nyingine alipokuwa ndani ya gari ya wagonjwa aliyotupiliwa ndani baada ya kukamatwa kwake katika uwanja wa ndege.

Wakili wake Robert Amsterdam amelaani hatua hiyo akisema Bobi Wine alikuwa na haki ya kutafuta matibabu ulaya.

Ripoti za hapo mwanzo ziliashiria alitekwa nyara kikatili na maafisa wa polisi wa Uganda waliovalia sare akatupiliwa katika ambulensi na kupelekwa mahali pasipojulikana.

Kukamatwa kwa mara ya pili kwa Bobi Wine na ambako hakukutarajiwa kulijiri takriban wiki moja baada ya kuachiliwa kutoka kizuizi chake kinyume na sheria na kulazwa katika hospitali ya Lubaga Kampala.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BOBI WINE AKAMATWA TENA, AZUILIWA KWENDA KUTIBIWA NJE BOBI WINE AKAMATWA TENA, AZUILIWA KWENDA KUTIBIWA NJE Reviewed by By News Reporter on 8/31/2018 12:26:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.