Loading...
Kwa wengi, mayai ni chakula kizuri kinachoweza kuliwa wakati wowote-asubuhi, mchana au jioni.
Isaac Nyamwamu, mkazi wa Roysambu, Nairobi hata hivyo amegundua njia ya kupata utamu zaidi kutoka kwa yai.
Huwa anayala pamoja na maganda yake. Mtandao mmoja wa habari wa nchini Kenya ulimtembelea nyumbani mwake kujua zaidi.
Tulimkuta mkewe akimwandalia chakula chake akipendacho. Sufuria ilikuwa imebandikwa juu ya jiko ikiwa na mayai 11.
Muda mfupi baadaye, ulikuwa ni wakati wa maankuli. Nyamwamu alieleza kuwa ulikuwa ni mwaka wake wa nane kula mayai na maganda yake.
"Nilianza kula mayai 2010. Marafiki na ndugu zangu walishangazwa na mtindo wangu mpya wa kula. Sikiweza kujizuia kula mayai kwa sababu yalikuwa tamu sana,” alisema.
Kila siku hupikiwa mayai saba na mkewe, “Kwa wakati mmoja nilienda kwa daktari kujua ikiwa maganda ya mayai yalikuwa na athari mbaya. Lakini aliniambia afya yangu ilikuwa nzuri,” alisema na kuongeza kuwa mayai hayo humpa ashiki za kimapenzi na kumfanya kuwa ‘pro’ kitandani.
Huwa anakula mayai hayo kwa ugali na kachumbari.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KUTANA NA MKENYA AMBAYE ANAKULA UGALI NA MAGANDA YA MAYAI, ADAI HUONGEZA NGUVU ZA KIUME
Reviewed by By News Reporter
on
9/01/2018 09:09:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: