Loading...
Mhubiri mmoja ameibuka na mafunzo tatanishi kwamba ni sawa kwa Wakristo ambao hawajafunga ndoa kushiriki mapenzi.
Hii ni kinyume kabisa na mafunzo ya Injili ambayo yanahimiza watu kutojihusisha na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.
Jarida la Christian Post lilimnukuu Romleigh McCleneghan akisema kuwa mtu yeyote hafai kuzuiwa kushiriki mapenzi iwapo hajaolewa.
McCleneghan anatetea msimamo wake akisema Wakristo hao makapera hawahitaji kujinyima mahaba kwa sababu unyoofu wa moyo ni kufanya mambo kwa kiasi.
Mhubiri huyo ambaye ameolewa na ni mama wa watoto watatu, amesema kuwa watu ambao hawajafunga ndoa wanaweza kuwa waaminifu katika uhusiano wowote wa kimapenzi ilmradi watazingatia kujidhibiti.
McCleneghan anasisitiza si sawa kuwataka Wakristo ambao bado hawajaolewa, na hawana maono ya kuishi kama watawa, kujinyima ngono ilhali wanaume kwa wanawake wote wanahitaji mapenzi.
Mafunzo ya mhubiri huyo ni kinyume kabisa na mafunzo ya Kikristo ambayo husisitiza watu kujizuia kushiriki ngono hadi watakapofunga ndoa.
Kushiriki mapenzi nje ya ndoa – mpango wa kando – ni dhambi itakayokusukuma katika moto wa milele.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

KUSHIRIKI NGONO KABLA YA NDOA NI SAHIHI, MHUBIRI ASEMA
Reviewed by By News Reporter
on
8/08/2018 11:03:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: