Loading...

MABASI YA SHULE YAGONGANA, MMOJA AFARIKI

Loading...
Basi la shule ya msingi Kivulini na la shule ya msingi Nyamuge ya mkoani Mwanza yamegongana leo asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Akizungumzia tukio hilo leo Agosti 23, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza(anayehamia makao makuu ya Polisi Dar,) Ahmed Msangi amesema aliyefariki ni dereva wa gari la shule ya Nyamuge Albert Joram(58).

Amesema watu wengine wanane na dereva wa  gari la Kivulini Kulwa Mayala 27, wamepata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao zaidi hasa miguuni.

“Majeruhi hao walikimbizwa katika kituo cha afya cha Buzuruga na baadae  mwanafunzi mmoja alilazimika kuhamishiwa hospitali ya rufaa, Bugando kwa matibabu zaidi huku wawili wakilazwa katika hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza,”amesema.

Amesema kwa sasa hali za majeruhi zinaendelea vizuri na tayari wale wa tano wameruhusiwa ingawa wanahitaji vipimo vya kina.
Na Lydia Mkeu.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MABASI YA SHULE YAGONGANA, MMOJA AFARIKI MABASI YA SHULE YAGONGANA, MMOJA AFARIKI Reviewed by By News Reporter on 8/23/2018 01:51:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.