Loading...

MAFURIKO INDIA: TAKRIBAN WATU 350 WAFARIKI, IKIWA 22,000 WAMEOKOLEWA

Loading...
Takribani watu 22,000 wameokolewa na mafuriko yaliyoikumba jimbo la Kerala, India siku ya jumapili, taarifa rasmi zimesema.

Kikosi cha jeshi na majanga na wavuvi walijitokeza katika uokoaji huo.

Helikopta pia zilifika kuhakikisha wananusuru maisha ya watu, kwa athari iliyoletwa na mvua kubwa iliyonyesha mfulululizo kwa wiki mbili.

Zaidi ya watu 350 wamefariki dunia, ikiwa wengi wao waliangukiwa na maporomoko ya ardhi, tangu kuanza kwa mvua hizo kali mwezi Juni.

Waziri mkuu wa jimbo la Kerala, Pinarayi Vijayan amesema idadi ya waanga imezidi kuongezeka na kufikia 725,000 kiasi ambacho kimezidi idadi stahiki katika kempu walizoandaliwa kuhifadhiwa waathiriwa hao.

Maeneo yaliyo athirika zaidi ni Chengannur, Alapuzha na Ernakulam. Vikosi vya uokoaji vinaendelea na kazi usiku na mchana kuhakikisha wananusuru maisha ya raia hao.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAFURIKO INDIA: TAKRIBAN WATU 350 WAFARIKI, IKIWA 22,000 WAMEOKOLEWA MAFURIKO INDIA: TAKRIBAN WATU 350 WAFARIKI, IKIWA 22,000 WAMEOKOLEWA Reviewed by By News Reporter on 8/20/2018 08:59:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.