Loading...

FILAMU LEO: 'CRAZY RICH ASIANS' YAVUNJA REKODI YA MAUZO

Loading...
Filamu ya Crazy Rich Asians imevuka matarajio katika rekodi za mauzo na umaarufu tangu uzinduzi wake mwisho juma lililopita.

Filamu iliyoandaliwa na watayarishaji maarufu duniani 'Warner Brothers' waliwachezesha Custance Wu na Henry Golding kama mastaa katika filamu hiyo ya kuchekesha ya kimapenzi ili kufanya vizuri chati za filamu.

Tangu kuzinduliwa kwake siku tano kupita, filamu hii - ambayo iligharimu dola za kimarekani $30 milioni - imekwisha tengeneza kiasi cha dola $34 milioni mpaka sasa.

Ni filamu ya kwanza Hollywood tangu 'The Joy Luck Club' miaka 25 iliyopita kuwatumia washiriki wenye asili ya Asia katika filamu nzima.

Crazy Rich Asians - Inamzungumzia msichana Rachel Chu na rafiki yake wa kiume, Nick machachari ambaye hakuwahi kufikiria kuwa familia yake ni tajiri.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
FILAMU LEO: 'CRAZY RICH ASIANS' YAVUNJA REKODI YA MAUZO FILAMU LEO: 'CRAZY RICH ASIANS' YAVUNJA REKODI YA MAUZO Reviewed by By News Reporter on 8/20/2018 09:32:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.