Loading...

WCB YATOA TAMKO MAVOKO KWENDA BASATA KUJISAJILI MARA YA PILI

Loading...
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameamua kujitoa rasmi katika Label yake iliyokuwa ikimsimamia ya WCB kwa ajili ya mgogoro wa mkataba aliopewa.

Baada ya kutoka WCB, Mavoko alionekana akienda kushtaki katika Baraza la Sanaa Tanzania ambapo pia alidaiwa kwenda BASATA kwa ajili ya kujisajili upya pamoja na kwamba alishasajiliwa chini ya WCB.

WCB wameibuka na kudai taarifa za Msanii huyo kwenda kujisajili BASATA sio sawa kwani tayari ameshasajiliwa chini ya Label hiyo mapema mwaka huu.

Kwenye mahojiano na mtandao mmoja habri, Meneja kutokea WCB, Sallam SK amesema hayo alipokuwa akieleza ushirikiano uliyipo kati ya WCB na Baraza hilo kwa sasa.

"Suala la kusema hatushirikiani na BASATA hilo litakuwa si la kweli na sisi tunashirikiana nao sana kuna vitu vinatokea bahati mbaya. Lakini ukiangalia wasanii wetu wote wamesajiliwa BASATA na hamna yeyote ambaye hajawahi kujisajili. Hata juzi kati hapa ilisemekana kuwa Rich Mavoko ndio alienda BASATA akajisajili, hapana!, kashasajili kupitia WCB, actually mwezi wa saba mwaka huu".
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WCB YATOA TAMKO MAVOKO KWENDA BASATA KUJISAJILI MARA YA PILI WCB YATOA TAMKO MAVOKO KWENDA BASATA KUJISAJILI MARA YA PILI Reviewed by By News Reporter on 8/20/2018 10:04:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.