Loading...

MOVIE LEO: MUIGIZAJI 'IDRIS ELBA' AGOMA KUCHEZA FILAMU ZA JAMES BOND

Loading...
Wakati dunia nzima ikiendelea kusubiri nani ambaye atamrithi muongozaji wa filamu ya Bond 25, tetesi kuhusu nani atafuata katika filamu zijazo za James Bond baada ya kutoka Daniel Craig zinazidi kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.

Kura za Uingereza zilizopigwa hivi karibu zimebaini Idris Elba ndio muigizaji anayefaa kucheza kama staa wa 007, katika filamu inayofuata, lakini kwa kujaribu kuwavunja moyo mashabiki hao kwa unyenyekevu, muigizaji huyo alizima uvumi huo na kudai yeye sio mtarajiwa na hatoigiza kama James Bond anayefuata.

Mtandao wa Good Morning Britain ulipata nafasi ya kumuuliza muigizaji, Elba maswali kuhusu swala la James Bond lakini ilipofika nafasi yake kuzungumzia swala hilo alisema: "Hapana" akiwa na maana hatokuwa muigizaji anayefuata katika muendelezo wa filamu za James Bond 007.

Filamu ya Bond 25 inatarajiwa kuzinduliwa Novemba 8, 2019, na ndio itakuwa filamu ya mwisho ya Daniel Craig lakini mpaka sasa bado haijajulikana ni nani atarithi nafasi yake ikiwa Elba amekataa.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MOVIE LEO: MUIGIZAJI 'IDRIS ELBA' AGOMA KUCHEZA FILAMU ZA JAMES BOND MOVIE LEO: MUIGIZAJI 'IDRIS ELBA' AGOMA KUCHEZA FILAMU ZA JAMES BOND Reviewed by By News Reporter on 8/23/2018 09:25:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.