Loading...
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amteua Emmanuel Ramazani Shadary kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo ifikapo Disemba 23 mwaka 2018.
Emmanuel Ramazani ni katibu wa chama tawala Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika mkutanao na waandishi wa habari msemaji wa serikali Lambert Mende Jumatano amefahamisha kuwa Rais Joseph Kabila amemteua Emmanuel Ramazani kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu nchini humo.
Kabla ya kuteuliwa kuwa mkombea katika uchaguzi huo, Shadary alikuwa naibu waziri mkuu alihusika na mambo ya ndani ikiwemo usalama.
Shadary ni mzawa wa Maniema , Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokria ya Kongo ambapo alikuwa gavana kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2001.
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

RAIS KABILA AMTEUA MRITHI WA KITI CHAKE
Reviewed by By News Reporter
on
8/10/2018 09:43:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: