Loading...
Rais wa Kenya apokelewa White House na rais Trump katika ziara yake rasmi nchini Marekani. Katika mazungumzo kati ya viongozi hao wawili, suala zima la ushirikiano katika sekta ya biashara na usalama ndio ambalo limezungumziwa.
Viongozi hao wamewaambia waandishi wa habari kuwa ushirikiano katika sekta ya biashara kati ya Marekani na Kenya unazidi kuimarishwa.
Akizungumza kuhusu Marekani kuwekeza nchini Kenya, rais Trump amesema kuwa kuna umuhimu pia wa ushirikiano katika sekta ya ulinzi.
Kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi, Trump amesema kuwa Kenya ni taifa muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi, hivyo basi Marekani haina budi kuzidisha ushirikiano wake na taifa hilo.
Na Paskali Joseph.Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS TRUMP NA KENYATTA WAJADILI UGAIDI NA BIASHARA MKUTANO WAO WHITE HOUSE, MAREKANI
Reviewed by By News Reporter
on
8/28/2018 11:29:00 AM
Rating:
![RAIS TRUMP NA KENYATTA WAJADILI UGAIDI NA BIASHARA MKUTANO WAO WHITE HOUSE, MAREKANI](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEih25x_6FuGVBCs8CySCbH7mKcxGy5J-WbFi1uuLPjbMhaq9mB9gOrTSIXsbIHNO7xZEkMm58SV_7xkEi4-Dcnpr-whphoUw1BCFt44wz2ndIv3wHldwyrcpKAt69jYDUwt_rlF89GMJMk/s72-c/ziara+ya+uhuru+kenya.jpg)
Hakuna maoni: