Loading...

VISA NA MIKASA: MCHUNGAJI AJARIBU KUMTAPELI MSHINDI WA JACKPOT, AKIONA CHAMTEMA KUNI

Loading...
Kulikuwa na kihoja katika kijiji kimoja Kathiani, Kaunti ya Machakos nchini Kenya wakati wakazi waliokuwa na ghadhabu walimshambulia mchungaji feki kwa mangumi na mateke kwa kumshutumu kwa jaribio la kumtapeli mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Mwanamume huyo aliyefahamika kwa jina David Maina Karimi kutoka kanisa la Chosen Church of Holy Spirit International, Kaunti ya Nyeri alifika katika kijiji cha Kathiani na kuomba kuonyeshwa njia ya kuelekea kwa mkazi aliyekuwa ameshinda Jackpot ya Sh33 milioni pesa za kikenya.

Karimi, ambaye alikuwa amevaa kilemba cheupe alidai kuwa alikuwa na ujumbe wake(mshindi wa Jackpot) kutoka kwa Mungu.

Alipofika, alimwambia mwanamume huyo kuwa Mungu alikuwa amemwambia atoe zaka ya asilimia 10 na amwongezee Sh 5 milioni pesa za Kenya.

Lakini waendeshaji wa bodaboda walitaka kujua jinsi alivyojua kuwa mshindi alitoka eneo la Kathiani kabla ya kumvamia, karibu wamuue.

Aliokolewa na polisi na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kathiani.
Na Geofrey Okechi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: MCHUNGAJI AJARIBU KUMTAPELI MSHINDI WA JACKPOT, AKIONA CHAMTEMA KUNI VISA NA MIKASA: MCHUNGAJI AJARIBU KUMTAPELI MSHINDI WA JACKPOT, AKIONA CHAMTEMA KUNI Reviewed by By News Reporter on 8/28/2018 11:10:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.