Loading...

TAMASHA LA KITALII PEMBA NA MASWALA YA MRENO

Loading...
Kisiwa cha Pemba hivi majuzi kiliandaa tamasha ya juma moja ambayo ilionyesha tamaduni za kuanzia tangu karne ya 16 wakati Ureno ilitawala visiwa vya eneo huilo.

Moja ya maonyesho hayo ni lile la kirumbizi - aina fulani ya densi au mapigano yenye chimbuko lake wakati wa mafunzo ya vita dhidi ya ukoloni wa Ureno.

Ureno ilitawala sehemu za pwani mwa nchi za Afrika Mashariki miaka ya 1500 na Zanzibar ilibaki sehemu ya himaya yake kwa karibu miaka 200.


Khamis Ali Juma, kutoka makavazi ya Pemba anasema kijiji cha Pujini ambapo tamasha hizo zilifanyika kilikuwa moja ya sehemu ambazo Wareno hao waliwasili kwanza.
Kupigana na fahali kuliletwa na Wareno na kuna tofauti na mfumo wa Wahispania kwa kuwa lengo kuu sio kumuua fahali bali kuwaburudisha watu.

Kuna imani kuwa tamaduni hii huchangia mavuno mazuri ya mpunga na hivyo tamaduni ya kupigana na fahali hufwanywa wakati wa kiangazia.
Pia kuna upande wa kimapenzi katika tamaduni ya kupigana na fahali ambapo wasichana huwashauri wapenzi wao wa kiume kushiriki ili kuonyesha ujasiri wao licha ya hilo kutofanywa saana kwa sasa.

Mwanamke anaweza kuchagua kanga mpya akajifunga na kuketi eneo fulani kutazama.

Ikiwa mpenzi wake atamaliza pigano bila kuumia atampa kanga ili aiweka kama zawadi.

Michezo inayowahusu punda kwenye vijiji vingi vya kisiwa cha Pemba pia ni suala muhimu kwenye sherehe.
Wale wanapanda punda huvaa kitamaduni na hubeba miavuli nyuma ya bendi.

Punda hutumiwa kwa uchukuzi na kilimo na uwepo wao kwenye tamasha hizo ni ishara ya umuhimu wao kisiwani. Miavuli pia huaminiwa kuvutia mvua.
Umbali huo wa kilomita 87 ni mgumu na waendesha baiskeli ni lazima wapitea aneo lenye mwinuko mkubwa zaidi kisiwani humo. Huwachukua washindani wengine zaidi ya saa mbili kukamilisha.

Kisha wao hukaribishwa kwenye ufukwe wa Vumawimbi kwa shangwe na nderemo.
Kwa kumalizia kuna mbio za mashua zinazojulikana kama ngalawa, Ngalawa ni mashua ambazo hutumiwa na wavuvi huko Zanzibar.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
TAMASHA LA KITALII PEMBA NA MASWALA YA MRENO TAMASHA LA KITALII PEMBA NA MASWALA YA MRENO Reviewed by By News Reporter on 8/14/2018 08:51:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.