Loading...

NGUO ZA KUBANA ZINAPUNGUZA NGUVU ZA UZAZI KWA WANAUME?

Loading...
Kuvaa nguo za ndani zilizo pana kunaweza kuwa njia rahisi kwa wanaume kuimarisha mbegu za kiume na homoni zinazozidhibiti, utafiti uliofanyika nchini Marekani umeeleza.

Utafiti uliowahusisha wanaume 656, uliofanywa na Chuo cha masuala ya afya cha Havard TH Chan nchini Marekani, wanaovaa boxer zilizo kubwa walikuwa na ongezeko kwa 25% ya ubora wa mbegu za kiume kuliko wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana.

Kutokuwepo kwa hali ya joto kwenye maungo ya kiume kunaweza kuwa sababu.

Wataalamu wanasema mtindo huu rahisi wa maisha unaweza kuboresha uzazi wa wanaume.

'Ubongo husaidia uzalishaji wa mbegu za kiume'
Uzalishaji wa mbegu za kiume haupendelei joto la zaidi ya nyuzi 34C, ndio maana korodani huning'nia kando ya mwili

Baadhi ya mitindo ya nguo za ndani, za kubana kama nguo za waendesha farasi, hubana maumbile hayo na kusababisha kutokea hali ya joto, huku mavazi ya ndani ambayo hayabani hufanya maumbile hayo kupata hewa ya kutosha.

Watafiti wamebaini kuwa wanaume wanaokwenda hospitali kwa ajili ya masuala ya uzazi wakiwa wamevaa nguo za ndani zisizobana wanakuwa ongezeko la ubora wa mbegu za kwa 17% .

Hata hivyo,maumbo ya mbegu hizo haziathiriwi wala ubora wa vinasaba vyake.

Pia watafiti walizingatia vitu kadha wa kadha ambavyo vinaweza kuathiri mbegu za kiume ikiwemo, Umri, uzito wa mwili na tabia kama kuvuta sigara, mazoea ya kutumia maji ya moto kwenye mabeseni ya kuogea vyote vinakisiwa kuwa joto lake linaweza kuwa chanzo cha tatizo.

Utafiti umebaini kuwa homoni zilizo kwenye ubongo zenye kazi ya kuziambia korodani kutengeneza mbegu za kiume, huitwa follicle stimulating hormone zilikuwa chini kwa 14% kwa wale wanaovaa nguo za ndani zisizobana.
Na Hamisi Fakhi.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
NGUO ZA KUBANA ZINAPUNGUZA NGUVU ZA UZAZI KWA WANAUME? NGUO ZA KUBANA ZINAPUNGUZA NGUVU ZA UZAZI KWA WANAUME? Reviewed by By News Reporter on 8/14/2018 09:01:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.