Loading...

VISA NA MIKASA: JAMAA AINGIA HOSPITALINI NA KUFANYA MAPENZI NA MKEWE ALIYELAZWA

Loading...
Mmiliki wa hoteli moja ya kifahari nchini Zimbabwe anaendelea kuhojiwa baada ya ripoti kutokea kuwa aliingia katika wadi ya kina mama hospitalini muda wa 9 usiku na kufanya mapenzi na mkewe aliyelazwa humo.

Jamaa huyo alifanya kitendo hicho hadharini mbele ya wagonjwa wengine 10 ambao pia walikuwa wakiendelea na matibabu.

Kabla kuingia humo, inadaiwa kuwa jamaa huyo alizozana na wauguzi wa hospitali hiyo waliomkataza kuingia ndani alipodai anataka kumuona mkewe. 

Kisa hicho kilithibitishwa na mkurugenzi wa matibabu hospitalini humo Amedeus Shamu ambaye alieleza kuwa uchunguzi unaendelea kubainisha ukweli.

''Ilikuwa muda wa saa 9usk ambapo baadhi ya wagonjwa katika wadi hiyo watoa ripoti kwa wauguzi kuwa kuna watu waliokuwa wakifanya tendo la ndoa katika wadi hiyo. Wauguzi hao waliwaarifu maaskari wa hospitali waliomtoa jamaa huyo upesi,’’ alisema.

Alipohojiwa na wauguzi, mwanamke huyo alieleza kuwa hangeweza kumzuia mumewe kufanya tendo hilo maana angempiga. 

''Singekataa kufanya mapenzi naye maana ningepigwa mbele ya wagonjwa, maana yeye hupenda vita sana,’’ mwanamke huyo alisema.
Na Fatma Pembe.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: JAMAA AINGIA HOSPITALINI NA KUFANYA MAPENZI NA MKEWE ALIYELAZWA VISA NA MIKASA: JAMAA AINGIA HOSPITALINI NA KUFANYA MAPENZI NA MKEWE ALIYELAZWA Reviewed by By News Reporter on 8/17/2018 10:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.