Loading...

VISA NA MIKASA: KANISA LAWAANDALIA WAUMINI WAKE POMBE WAKATI WA IBADA

Loading...
Kanisa la The Greater Purpose Community Church lililoko Marekani limesemekana huwa linawaandalia waumini wake pombe ya aina ya bia na mvinyo wakati ibada inapokuwa ikiendelea.

Kanisa hilo ambalo lilikuwa kule Santa Cruz mjini California, limeripotiwa kuhamia katika makao yake makuu ambapo pombe inatiririka kwenye mifereji. 

"Hakuna popote kwenye Biblia ambapo pameandikwa huwezi kunywa pombe katika hali ya kuwajibika," Chris VanHall, mhubiri wa kanisa hilo alisema.

VanHall alisema kuwa pombe imekuwepo katika makanisa tangu karne zilizopita na hata wanapanga kufungua kampuni yao binafsi ya kutengeneza pombe hivi karibuni. 

"Bia ni kinywaji ambacho hutumika sana katika jamii, utapoinywa katika hali ya kuwajibika inaweza leta watu pamoja kupitia njia ambazo ibada za kitamaduni haziwezi," VanHall aliongezea.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: KANISA LAWAANDALIA WAUMINI WAKE POMBE WAKATI WA IBADA VISA NA MIKASA: KANISA LAWAANDALIA WAUMINI WAKE POMBE WAKATI WA IBADA Reviewed by By News Reporter on 8/17/2018 10:55:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.