Loading...
Polisi jijini Nairobi wameanzisha msako kumkamata mwanamke aliyemkata mume wake sehemu za siri katika mtaa wa mabanda wa Mukuru mnamo Alhamisi, Agosti 24.
Esther Namale anadaiwa kumvamia mume wake Godfrey Namale, aliyeingia nyumbani akiwa mlevi na kuingia kitandani.
Kulingana na ripoti ya gazeti la Nation, wawili hao wameishi pamoja miaka 20, na wana watoto wawili.
“Baada ya kazi nilikwenda kunywa kidogo kabla ya kurejea nyumbani kulala.
"Mara nikasikia uchungu mwingi katika sehemu zangu za siri na baadaye nikaona damu ikitiririka. Mke wangu alikuwa amesimama kando yangu na kisu mkononi,” alisema.
Kisha alichukua jukumu la kwenda kwa mwenyekiti wa kijiji Ibrahim Mohammed ambaye alimkimbiza hospitali ya Crescent na kisha kuripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Industrial Area.
Kwa sasa polisi wanamsaka mama huyo ili kumchukulia hatua za sheria na mume wake kupata haki.
Na Mary Mkeu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: MAMA MMOJA AFYEKA NYETI ZA BABA NA KUTOROKO, ASAKWA NA POLISI
Reviewed by By News Reporter
on
8/26/2018 11:31:00 AM
Rating:
![VISA NA MIKASA: MAMA MMOJA AFYEKA NYETI ZA BABA NA KUTOROKO, ASAKWA NA POLISI](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhe3ubgu3xuA4IOr6d9dGcKogG83ky5r0dmROYcGVXPGn23LmOKq_VLi_W5sy3KXamqGQVm03bNIUjg7eVOGwckaXmQvIFc35pzYSRaTCyUk0vM3ax-pewajGZPp4mG-Ii74H9HeNipwXE/s72-c/baba+aliyekatwa+nyeti+zake.jpg)
Hakuna maoni: