Loading...
Watanzania wengi wameanza kuviasi vyakula vya kiasili na kupendelea sana kula vyakula vya kizungu ambavyo vina madhara chungu mzima kwa afya.
Kwa kawaida, mwanadamu huitaji kalori 2200 vipimo vya nguvu na gramu 2000 za chumvi kulingana na wataalam wa afya, lakini vyakula vya siku hizi vimejaa sukari, mafuta na chumvi ambavyo vina madhara mengi na maradhi. Chanzo chake ikiwa ni uwezo mkubwa wa kifedha na pia ari ya kupanda ngazi kimaisha. Vifuatavyo ni vyakula hatari kuepukana navyo:
1. Chipsi (Zege)
Katika lugha za mitaani hujulikana kama kiepe. Kisahani kimoja cha chipsi huwa na takriban 260mg ya chumvi, kalori 400 na kiasi cha mafuta gramu 216, zinazidisha unene usio wa kawaida yaani kitaalam Obesity. Kwa kawaida, mtu mwenye afya njema hula vipimo vya 2000 mg vya chumvi kwa siku.
Lakini, ukiwa na shida za shinikizo la damu au uzito kupita kiasi katika umri wa miaka hamsini na zaidi, punguza ulaji wa chumvi hadi miligramu 1500 kwa siku. Chumvi nyingi hulowesha mwili na hivyo kuupa moyo wakati mgumu unaposhinikiza damu kwenye mishipa.
Polepole moyo hufifia na hivyo kuongeza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo. Lakini, ilikuyaepuka magonjwa haya, chipsi vyaweza pikwa vizuri. Badala ya kuvitumbukiza ndani ya mafuta, waweza tumia mafuta kidogo kwa kukarangia na kuchanganya na mboga kiasi wakati unapokula.
2. Nyama ya Kusindika
Nyama za kusindika huwekwa kemikali ili kuzipa muda mrefu bila kuharibika. Vyakula hivi ni kama Bacon, sausages, Salami na Sandwich Browns na vinginevyo. Vyakula hivi huhusishwa na magonjwa kama Saratani na magonjwa ya moyo.
Kulingana na utafiti uliofanywa mwaka wa 2010 na chuo kikuu cha Harvard kuhusiana na afya ya umma, ilibainika kuwa nyama za kusindika huchangia kwa asilimia arobani na mbili ya magonjwa ya moyo, na asilimia kumi na tisa kwa aina ya ugonjwa wa kisukari (Diabetes 2). Kemikali inayotumika kuzihifadhi huharibu mishipa ya damu na hivyo kuchangia magonjwa mengi ya moyo.
3. Kuku wa kukaanga
Mafuta mengi yapatikanayo kwa kuku za kutumbukiza kwa mafuta huchangia pakubwa kwa ugonjwa kisukari, magonjwa ya moyo na aina fulani za saratani.
Kwa sababu ya vipimo vya juu vya moto ambavyo hutumika kuvipikia, madini muhimu huchomeka na kuisha hivyo basi kuondoa virutubishi vya maana. Pia hukaushwa na kuwa ngumu kusagika.
Robo kuku huwa na Kalori 534, gramu 31 za mafuta, na 550mg za chumvi. Kuku huwa na madini mengi kwani ni kati ya nyama zingine nyeupe ambazo hushambikiwa sana kuwa zenye afya. Hivyo, ikipikwa vizuri kwa kukaanga kwa mafuta kiasi, itakuwa tamu na yenye afya.
4. Nyama choma
Nyama inapopikwa kwa njia ya kuchoma, mafuta ya nyama hudondoka na kuanguka kwa makaa moto. Moshi utokao hapo huwa na kemikali iletayo saratani ya matumbo na nyungu ya choo. Pia watu wengi hupendelea kula nyama choma wanywapo pombe. Hii huchangia ugonjwa wa misuli (Gouts). Ili kuepuka madhara hayo, ni vizuri uchemshe nyama au kukaanga kwa mafuta kiasi.
5. Tambi
Tambi ni vyakula vitokavyo kwa nafaka mbali mbali. Hukaushwa na kuwekwa. Hivi vyakula huwa na kiwango cha chini cha madini. Kemikali zinazotumika kuongeza muda wa kukaa na pia kuzifanya ziwe nzuri, huleta shida za shinikizo la damu (blood pressure) na shida za figo.
6. Soda
Soda hutumika sana kukomesha kiu na kuburudisha. Lakini, kwa kila chupa ya soda unywapo, wajua kuwa huwa umetumia takriban vijiko kumi vya sukari? Hii uongeza kiwango cha sukari kwa mwili na hivyo huchangia ongezeko la shinikizo la damu , kisukari na pia upungufu wa madini muhmu mwilini.
7. Pombe
Pombe huhusishwa na magonjwa hatari moyo kama vile shinikizo la damu na kiharusi (Stroke).
Pia hususishwa na magonjwa mengine kama vile shida za ini, na saratani.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VYAKULA 7 AMBAVYO HUSTAHILI KULA KWA WINGI
Reviewed by By News Reporter
on
8/26/2018 12:10:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: