Loading...

BOT YAPUNGUZA RIBA TENA, WAKOPAJI WAULA

Loading...
Wananchi wa kawaida na wafanyakazi watapata ahueni ya kukopa katika benki mbalimbali nchini huku riba zikitarajiwa kupunguzwa tena na muda wa kurudisha mikopo kuongezwa.

Ni dhahiri kuwa sasa wafanyabiashara wadogo, wananchi wa kawaida, wafanyakazi na sekta binafsi za biashara zitapata fursa ya kukopa na sifa ya kukopesheka baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)kupunguza riba kwa benki nchini kutoka asilimia tisa hadi saba.

Punguzo hilo la riba linazipa benki fursa ya kukopa na kurudisha kwa riba ndogo zaidi.

Suala hilo linaweza kusababisha mwananchi wa kawaida kuwa na sifa ya kukopesheka katika benki, kurudisha kwa muda mrefu kwa riba ndogo.

Punguzo hilo la riba litaanza rasmi Agosti 27 na litaendelea hadi yatakapofanyika mapitio mapya.

Ndani ya mwaka mmoja na nusu, BoT imeshuka kwa zaidi ya nusu riba ya mikopo hivyo kuzishawishi benki za biashara nazo kufanya hivyo na kuwapa unafuu wananchi wachache wanaonufaika moja kwa moja na sekta ya fedha nchini.

Machi mwaka jana, BoT ilishusha riba kwa asilimia nne kutoka asilimia 16 mpaka asilimia 12. Agosti mwaka huo huo ikashusha tena mpaka asilimia tisa iliyodumu mpaka sasa.

Uamuzi huo unakusudia kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wananchi na sekta binafsi ili kufanikisha sera ya uchumi wa viwanda inayopewa kipaumbele na Serikali.
Na Neema Joshua.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BOT YAPUNGUZA RIBA TENA, WAKOPAJI WAULA BOT YAPUNGUZA RIBA TENA, WAKOPAJI WAULA Reviewed by By News Reporter on 8/26/2018 12:41:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.