Loading...
Wakati wakazi wa Kata ya Maanga Jijini Mbeya wakiendelea na upigaji kura wa kumchagua diwani wa kata hiyo leo Septemba 16, mkazi wa eneo hilo Elizabeth Mwambipile ameamua kushusha neno la Mungu akiombea uchaguzi huo ufanyike kwa amani na utulivu.
Mwanamke huyo akiwa amepanga foleni wenzake katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Maanga, amejikuta akianza kuhubiri neno la Mungu akiombea amani ya uchaguzi huo.
'Eeeh! Yehova tunajikabidhi mikononi mwako, tunaomba uchaguzi uwe wa amani na utulivu. Roho mtakatifu simamia kura, roho za shetani, mapepo tuzifute kwa jina la Yesu Kristo, amina,” amesikika mama huyo.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika kata hiyo, Upendo Mtenzi amesema licha ya kujitokeza changamoto ndogondogo, lakini wananchi wanaendelea kupiga kura katika vituo vyote 15 vya kata hiyo.
Amesema, “Kweli kulikuwa na changamoto kidogo, kama vile mawakala walikuwa wabishi, walitaka waanze kuhakiki daftari zima la wapiga kura kabla ya kuanza kupiga kura, lakini hilo tumeliweka sawa na wanaendelea vizuri hadi sasa.”
Wakati huohuo, ulinzi umeimarishwa kila kona la kata hiyo, magari yakiwa na askari yanapiga doria.
Mbali na askari hao wanaozunguka mitaani na walioko kwenye vituo, lakini pia kuna walinzi wa vyama vya CCM na Chadema ambao wanafuatana fuatana na wengine wamepiga kambi karibu na vituo vya kupigia kura.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

AENDESHA IBADA KITUO CHA KUPIGIA KURA
Reviewed by By News Reporter
on
9/16/2018 10:20:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: