Loading...
Familia ya Kenya iishio Marekani inaomboleza baada ya baba wa familia kumkanyaga mtoto wao wa kiume wa miezi 18 hadi kufa alipokuwa akiendesha gari kinyumenyume katika maegesho yao mnamo Jumatatu, Septemba 10.
Mtoto huyo, Mishael Mutuma, jinsi ilivyoripotiwa aliondoka nyumbani na kutembea bila kugunduliwa nyuma ya gari wakati babake Dan Mutuma, muuguzi katika Kansas City, alipomkanyaga.
Kulingana na ripoti ya Fox 4 News, Mutuma alikuwa amerudi nyumbani kuchukua stakabadhi fulani alizokuwa amesahau alipokuwa akielekea chuoni anaposomea.
Alichukua stakabadhi hizo kwa haraka, akamuaga mkewe Loise, aliyekuwa akiwatunza mapacha wake na mama mkwe wake, na kuondoka nyumbani wakati tukio hilo la kuhuzunisha lilipotokea.
Aidha, iliripotiwa polisi wa eneo hilo Olathe wanachunguza kisa hicho lakini hawatawasilisha mashtaka yoyote ya uhalifu kutokana na kisa hicho wanachokichukulia kama ajali.
Mtoto huyo anaripotiwa kuwa ni mjukuu wake Pasta Moses Mutuma wa kanisa la Miathene Seventh Day Adventist (SDA) kaunti ya Meru County.
Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

INAHUZUNISHA, BABA AMUUA MTOTO WAKE KIKATILI
Reviewed by By News Reporter
on
9/16/2018 11:01:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: