Loading...
Jamii ya Becheve iishiyo milimani katika makutano ya mto, wasichana wadogo hutumiwa kama sarafu, kubadilishana kwa chakula na pesa.
Watu wa mji huo huita desturi hiyo, "Fedha Mwanamke Ndoa".
Kabila la Becheve linajumuisha makabila 17 madogo madogo ambayo yanaishi katika eneo la milima ya Obanliku chini ya serikali ya mtaa ya jimbo la Cross River, Nigeria, eneo ambalo pia ni nyumba ya kivutio cha zamani cha utalii, Obudu Cattle Ranch.
Kwa pamoja makabila haya huendeleza mila za kale ambapo wasichana wadogo hutolewa kama "wake fedha", wakati mwingine hata kabla hawajazaliwa, kwa mbadala wa kiasi fulani au kukidhi deni la awali.
Wake hawa kimsingi hukabidhiwa kwa waume zao kama bidhaa, ili kuleta amani, wakati familia inafurahia ulipwaji wa deni na kuendelea kupata faida fulani.
Mara nyingine, ndugu wa mwanamke huendelea kumtembelea mume wa binti yao kuchukua zawadi na pesa.
Mbali na mkuu wa familia (Baba) ambaye alimuozesha binti yake kwa ndoa ya pesa, ndugu wa mama wa binti huyo wapo huru kwenda kukusanya vitu kutoka kwa 'mkwe wao'. Kitu chochote kilichotolewa wakati wa ziara yao kinapewa thamani ya fedha na kuwekwa katika kumbukumbu na mkwe wao.
Wasichana hawana sauti katika maamuzi hayo. Makubaliano mara nyingi ufanywa wakati akiwa mchanga. Baadhi yao kuuza hata kabla hawajazaliwa.
Wasichana hao mara nyingi huathiriwa kisaikolojia na kimwili pia.
Kutokana na mila na desturi hizo za kale katika jamii hiyo inavyoendelea na hata kutoa matokeo hasi dhidi ya mabinti wa jamii hiyo ya Becheve serikali ya eneo hilo imeshaanza kuchukua hatua za makusudi ili kuhakikisha vitendo hivyo vya kinyanyasaji.
Na Mike Petro.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

JAMII INAYOOZESHA MABINTI ILI KULIPA DENI
Reviewed by By News Reporter
on
9/17/2018 12:30:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: