Loading...
Fikiria kuwa na ulemavu wa macho (kipofu), umebakwa, sambamba na kupata ujauzito na baada ya kujifungua, unakuja kujua wewe na mwanao kichanga mmepata maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU).
Hii si hadithi iliyosimuliwa katika filamu, ni stori ya kusikitisha ya mwanamke, 44, mwenye upofu wa macho, Hajara Laila, ambaye alibakwa na mtu asiyejulikana miezi kadhaa iliyopita jijini Accra, Ghana.
Hajara Laila alishuhudia kisanga chake cha kusikitisha kwa mwanahabari wa wa mtandao wa GHOne News bi. Alice Aryeetey.
Kwa zaidi ya miaka 30, Laila mwenye umri wa miaka 44 amekuwa na ulemavu wa macho.
Laila alipata upofu wa macho akiwa na umri kati ya miaka 10 mpaka 11 baada ya kupatwa na maambukizi ya macho, ambapo ugonjwa huo wanauita "apolo" kwa asili ya kwao, lakini mama yake, ambaye pia alipata upofu siku sita kabla ya kuzaliwa kwake, alishindwa kumsaidia.
Ingawa maisha hayakuwa yenye furaha, maisha yake yalikuwa yenye maana, mpaka siku hiyo ya kutisha na ya bahati mbaya ilipofika, pale alipobakwa na mtu aliyeshindwa kumtambua.
Mtu asiyejulikana alimlazimisha kufanya ngono kwa nguvu. "Sikwenda hospitalini baada ya tukio hilo kwa sababu sikufikiria kama ningeshika uja uzito, lakini hata baada ya kutambua nilikuwa na mimba, Sikutaka kutoa mimba ya kiumbe asiye na hatia na sikuweza kujua nani alihusika," alisema Laila.
Kulingana na Laila, miezi miwili baada ya tukio la ubakaji, aliona mabadiliko fulani katika mwili wake na alifika hospitalini kwa uchunguzi; na alijikuta ameambukizwa VVU na ni mja mzito.
Laila amethibitisha kwamba ameambukizwa virusi na aliye mbaka kwa kuwa huko nyumba hakuwa kuonekana anamaambukizi hayo.
Wiki mbili zilizopita, alijifungua mtoto wa kike, ambaye kwa bahati mbaya naye alikuwa ameambukizwa VVU.
Wataalamu wa afya wameonyesha kuwa VVU vinaweza kuenea kutoka kwa mama hadi kwa mtoto wakati wa ujauzito - kupitia placenta au wakati wa kwakunyonyesha.
Ingawa kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito lakini Laila hakujua mapema kama ni mjamzito katika hatua ya mwanzo na kujikuta kuanza tiba wakati ambapo mtoto alikuwa ameambukizwa.
Akifuta machozi, alisema kuwa alikuwa akiomba msaada kwenye magari na alikuwa mwanachama wa bendi ya kuimba ya walemavu ili kuendesha maisha yake.
Lakini sasa, ilimbidi asimame na akae nyumbani ili amuhudumie mwanae na yeye mwenyewe, kwa shida zisizopimika.
"Maisha yamekuwa magumu kwangu kwa sababu sijawahi kuwa na amani wala furaha katika maisha yangu yote. Yule ambaye angeweza kunisaidia ni mama yangu ni kofu na hanauwezo. Chakula, mavazi na sehemu ya kuishi ni duni, hata ninapoishi sasa si salama," Laila alisema kwa uchungu.
Takribani wanawake sita wanaweza kubakwa kila wiki, kulingana na takwimu za miaka sita kutoka katika kitengo cha Uhalifu cha nchini Ghana iliyotolewa mwaka 2017.
Kiwango cha uhalifu nchini kote, kwa mujibu wa Idara ya Uchaguzi wa Uhalifu wa Polisi ya Ghana (CID) pia iliongezeka kwa kiasi kidogo katika robo ya kwanza ya 2018.
Takwimu hizi za kushangaza na hadidhi ya kusikitisha ya Laila, Serikali inajipanga kuchukua hatua madhubuti juu vitendo vya kiovu wanavyofanyiwa walemavu katika makundi mbali mbali.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

INAHUZUNISHA; MLEMAVU ABAKWA, ATIWA MIMBA, AAMBUKIZWA VVU
Reviewed by By News Reporter
on
9/17/2018 03:26:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: