Loading...
Nairobi ni mji tajiri zaidi Afrika Mashariki na wa sita Afrika baada ya Durban, Cape Town, Cairo, Lagos na Johannesburg, kulingana ripoti ya New World Wealth na AfrAsia Bank kutoka Mauritius.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa utajiri wa jiji la Nairobi unakadiriwa kuwa Sh5.4 trilioni na matokeo ya ukuaji huo unatokana hasa na shughuli za huduma za kifedha, biashara za rejareja, utalii, huduma za mawasilino, ujenzi na kupangisha majengo.
Nairobi huvutia matajiri kuwekeza na kufanya biashara wakati mji wa pwani ya Kenya, Mombasa umetajwa kama nyumbani kwa watalii na wawekezaji wa anasa pamoja na majumba yake ya kihistoria yanayotambuliwa kama maeneo ya urithi wa Dunia.
Ripoti hiyo ilionyesha pia kuwa Mombasa ina uwekezaji wenye thamani ya Sh80 bilioni, hasa katika mahoteli na majumba ya starehe.
Ripoti hiyo inaonyesha matajiri wa Afrika Mashariki wanapenda kununua nguo, huku wakenya wakimiliki magari ya kifahari kama porsche na kuna mwenendo mpya umeingia kwa Wakenya kupenda kumiliki helikopta na ndege binafsi.
Jiji la Dar Es Salaam ambalo linaiwakilisha Tanzania haijaachwa mbali na Nairobi yenyewe kuwa na jumla ya utajiri wa Sh2.5 trilioni, ikifuatiwa na Kampala ya Uganda ambayo nayo inajumla ya utajiri wa Sh1.6 trilioni.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

NAIROBI YATAJWA KAMA JIJI TAJIRI AFRIKA MASHARIKI, DAR YAMFUATIA
Reviewed by By News Reporter
on
9/17/2018 04:55:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: