Loading...

KAMBA MKUBWA ZAIDI ANAPATIKANA TANZANIA

Loading...
Kamba Nazi (Birgus latro), pia anaitwa Kamba kabali, ana urefu wa sentimita 45 ni moja kati ya kamba wakubwa waishio nchi kavu. Jina lake linatokana na uwezo wa kamba hao kupanda miti ya minazi na kuangua nazi au madafu, ambacho ndio chakula wakipendacho.

Kamba hao uzaliwa majini kisha hubadilika na kuishi nchi kavu, pia urudi majini wakiwa wakubwa kwa ajili ya kutaga mayai.

Kwa bahati mbaya, kaa nazi huwindwa kwa utamu wa nyama zao, na hii kuzidi kufanya wazidi kupungua na kuwa wachache. Wanapatikana Zanzibar pekee dunia nzima katika kisiwa cha Chumbe.

Mbali na uwezo wake wa kuangua madafu kama chakula chake pendwa, pia ana uwezo wa kuwinda ndege kadhaa wanaotafuta chakula chao baharini.

Kutokana na kuwa adimu mpaka wamefikia kutojulikana kwa idadi yao kamili ila kwa sasa inakadiriwa wapo zaidi ya 300.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KAMBA MKUBWA ZAIDI ANAPATIKANA TANZANIA KAMBA MKUBWA ZAIDI ANAPATIKANA TANZANIA Reviewed by By News Reporter on 9/17/2018 05:43:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.