Loading...

BEI ELEKEZI YA KOROSHO YATANGAZWA,WAKULIMA KUNEEMEKA

Kamati ya bei elekezi iliyokutana mkoani Mtwara imepitisha bei dira ya korosho kwa mwaka 2018/2019 kuwa ni shilingi 1550 kwa daraja la kwanza na Tsh 1240 daraja la 2.

Kamati hiyo iliyojumuisha uwakilishi wa wajumbe kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendele, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, vyama vikuu vya ushirika, washauri wa kilimo, warajisi wasaidizi wa Mikoa, wakulima kutoka mikoa inayolima zao korosho kwa wingi, pamoja na bodi ya korosho Tanzania kwa pamoja wafikia makunbaliano hayo kwa kuzingatia tafiti zilizofanyika.

Kwa kuzingatia taarifa kutoka kwa wataalam wa taasisi ya utafiti wa kilimo Naliendeele iliyowasilishwa mbele ya kamati iliyoonesha gharama za uzalishaji wa korosho ghafi kwa kilo moja katika mazingira ya mkulima msimu 2017/2018 ilikuwa ni shiilingi 1,291.89 bila ongezeko la faida ya asilimia 20.

Aidha asilimia 20 kama faida ya
Loading...
gharama za uzalishaji kilo moja ya korosho ghafi ni shilingi 258.38, hivyo gharama halisi ya uzallishaji ni pamoja na asilimia 20 kama faida kwa kilo moja ya korosho ghafi ni kiasi cha shilingi 1,550.

Hivyo kutoka na taarifa hiyo wajumbe wamekubaliana na kupitisha bei elekezi kwa msimu wa mwaka 2018/2019 kuwa ni kiasi cha shilingi 1550.00

Itakumbukwa kuwa msimu uliopita bei elekezi ilikuwa 1450 (daraja kwanza na 1160 daraja la pili) na Wanunuzi kwenye minada walinunua hadi Tsh 4000 kwa kilo, ndio maana inaaminika kuna asilimia kubwa ya bei kupanda msimu huu.

Kwa kawaida Mnunuzi haruhusiwa kununua chini ya bei elekezi..hivyo kwa bei hii kuna asilimia kubwa ya bei kwenye minada Kupanda zaidi ya msimu uliopita.
Na Peter Godwin.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BEI ELEKEZI YA KOROSHO YATANGAZWA,WAKULIMA KUNEEMEKA BEI ELEKEZI YA KOROSHO YATANGAZWA,WAKULIMA KUNEEMEKA Reviewed by By News Reporter on 9/29/2018 10:20:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.