Loading...

MUSEVENI AGOMEA ONGEZEKO LA MISHAHARA

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezuia ongezeko la posho na mishahara kwa watumishi wa umma.

Hapo awali ongezeko lilifanyika Juni 2018. Baraza la Mawaziri hatimaye lilikubali viwango vipya vya mishahara na posho kwa sababu viwango vya hapo awali vilikuwa "haviridhishi" kutokana na gharama za maisha kuongezeka.

Hata hivyo, uamuzi huo haukwenda vizuri baada rais Museveni kumwagiza Waziri Mkuu, Dkt. Ruhakana Rugunda kwa barua ya Agosti 30, 2018, kuitisha mkutano wa Baraza la Mawaziri mapema mwezi huu, ili kugeuza uamuzi huo.
Loading...
if;">
Rais Museveni alihoji Baraza hilo kwa nini walikubali kupitisha uamuzi huo baada ya bajeti ya serikali kupitishwa na huku wakijua kuwa hakuna pesa za ziada za kutekeleza uamuzi huo katika bajeti elekezi ya mwaka 2018/19.

Katika uamuzi wa ongezeko la posho na mishahara uligusa hasa viongozi wa juu wa nchi kama waziri mkuu, makamo wa rais na viongozi wengine wa ngazi za juu za serikali.

Baada ya agizo hilo la rais Museveni msemaji wa serikali alitangaza mapema mabadiliko hayo yaliyopendekezwa na rais kwa umma wote.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MUSEVENI AGOMEA ONGEZEKO LA MISHAHARA MUSEVENI AGOMEA ONGEZEKO LA MISHAHARA Reviewed by By News Reporter on 9/29/2018 01:21:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.