Loading...

BEYONCE ASHTAKIWA KWA USHIRIKINA

Loading...
MWANADADA aliyekuwa mpiga ngoma wa muimbaji Beyonce, Kimberly Thompson, amemshtaki msanii huyo kwa kutumia uchawi kupita kiasi.

Kimberly ameeleza kuwa alifanya kazi katika bendi ya Beyonce kwa zaidi ya miaka saba kama mpiga ngoma.

Kulingana na stakabadhi za mlalamikaji, Kimberly anadai kuwa Beyonce alitumia ushirikina kumdhalilisha, kumnyanyasa kimapenzi na hata kuwasumbua wapenzi wake.

Aidha, Kimberly amedai kuwa Beyonce alimuua mbwa wake japo hakuweza kudhibitisha.

Ombi lake la kutoka Beyonce kuchunguzwa kuhusu ushirikina lilikataliwa kortini hapo huku jaji akidai kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha.

Kimberly amefanikiwa kuzindua albamu zake nne baada ya 'Kutengana' na Beyonce

Katika ripoti za awali, dansa mmoja wa Beyonce raia wa Nigeria alieleza kuhusu namna walivyomuokoa msanii huyo kwa shabiki wake aliyekasirika alipotaka kumvamia akitumbuiza jukwaani.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
BEYONCE ASHTAKIWA KWA USHIRIKINA BEYONCE ASHTAKIWA KWA USHIRIKINA Reviewed by By News Reporter on 9/22/2018 11:01:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.