Loading...
JESHI la Polisi Dar es Salaam linamshikilia msanii wa Bongo Fleva, Faidha Omary ‘Sister Fey’ kwa kosa la kukiuka maadili kwa kuchapisha maudhui yanayodhalilisha kwenye mitandao ya kijamii.
Fey amekamatwa kwa amri ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ambaye amesema kuwa aliiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kumfuatilia msanii huyo juu ya matumizi yake ya mitandao na hatimaye alikamatwa Septemba 19, 2018 usiku na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama na sasa anasubiliwa kufikishwa Mahakamani
Shonza amesema alitegemea huenda Fey angebadilika mwenendo wa tabia yake hiyo, baada ya kuitwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa mara ya kwanza badala yake alizidisha kuchapisha picha na video hizo kinyume cha sheria ya makosa ya mitandao.
Fey amekuwa akichapisha picha na video tofauti tofauti hasa kwenye ukurasa wake wa Instagram zikimwonyesha akiwa kwenye mahaba mazito na mpenzi wake ‘kibenteni’.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

SISTA FEY MBARONI KWA MAKOSA YA MTANDAO
Reviewed by By News Reporter
on
9/22/2018 11:26:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: