Loading...
Ingawa hakuna jipya duniani, lakini kuna baadhi ya visanga ukisimuliwa vinashangaza.
Kuna kisanga kimoja kimetokea huko Uganda ambapo joka kubwa 'lilimkamata' na kumuweka kizuizini jamaa mmoja mpaka alipokamatwa rasmi na polisi kwa shutuma ya wizi.
Mwanaume huyo alikuwa ameiba katika eneo la Kyenjojo, eneo la magharibi mwa Uganda.
Mwanaume huyo aliiba godoro majira ya asubuhi siku hiyo, lakini alipokuwa akiondoka, joka kubwa lilimvamia na kujizungusha shingoni mwake.
Mwanaume huyo aliyekuwa akijaribu kukimbia na godoro hilo, hakuwa na la ziada zaidi ya kupiga kelele za kuomba msaada wa kuokolewa.
Watu kadhaa waliosikia kilio chake walikimbia kumsaidia, lakini hakuna aliyethubutu kufanya chochote kwa kuhofia joka hilo polisi.
Mganga wa kienyeji aliitwa ili kumuokoa mwanaume huyo lakini hata yeye alishindwa. Kisa hicho kilichapishwa katika mitandao ya kijamii ya Uganda na hatimaye taarifa hiyo kuenea kote.
Na Mary Mkeu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

JOKA LA AJABU LAMKAMATA MWIZI WA GODORO
Reviewed by By News Reporter
on
9/22/2018 11:53:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: