Loading...
Meneja wa klabu ya Yanga ambaye ni mchezaji aliyestaafu mwaka huu kuichezea klabu hiyo, Nadir Haroub Cannavaro amezungumzia adhabu iliyotolewa na TFF kwa meneja wa klabu ya Simba, Robert Richard hapo jana.
Meneja huyo wa Simba amefungiwa kwa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana na kuihujumu timu ya taifa na kutotii maagizo ya TFF yaliyopelekea wachezaji sita wa klabu hiyo kuondolewa katika listi ya timu ya taifa.
Akizungumza na EATV moja kwa moja kutoka katika mazoezi ya klabu hiyo, Cannavaro amesema,
"Kwa upande wangu mimi siwezi kulizungumzia sana hilo kwasababu sijui tatizo lilikuwa wapi na sijui ni muda gani alipata taarifa ya kwamba wachezaji wanahitajika kambini, TFF wao ndiyo wanajua ukweli wake ndiyo maana wamelitolea maamuzi".
"Lakini kwangu mimi niliwasiliana na Katibu Mkuu wa TFF, akaniagiza kuwa wachezaji wakirejea kutoka kwenye mchezo wao nchini Rwanda wawasili kambini mara moja na nilitekeleza hilo. Na kuhusu suala la Feisal Salum tulishaliongea na uongozi wa TFF tukalimalizana kwahiyo Yanga haina matatizo tena na TFF", ameongeza Cannavaro.
Aidha, meneja huyo wa klabu ya Yanga amesema wamechukua hatua kwa mchezaji wao, Feisal Salum ambaye alikumbwa na sakata hilo la kuondoshwa katika listi ya timu ya taifa kwa kumpa elimu zaidi kuwa endapo kambi ya timu ya taifa itakapotangazwa anatakiwa awasili kambini kwa wakati.
Na Mary Mkeu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
CANNAVARO AZUNGUMZIA KUFUNGIWA KWA MENEJA WA SIMBA SC
Reviewed by By News Reporter
on
9/11/2018 04:30:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: