Loading...
Polisi mjini Nakuru - Kenya, wanamshikilia mwanamke mwenye umri wa makamo aliyedaiwa kujaribu kumuuza mwanae wa umri wa wiki tatu baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani kutoka katika hospitali ya Nakuru Level Five.
Anne Wangui, 35, ambaye ni mkazi wa Njoro alisema kuwa alijaribu kumuuza mwanae kwa Dorcas Nanjala kwa Sh. 27,000 bila kufanikiwa.
Mteja wa Wangui alikuwa amempoteza mtoto wake wakati alipopata soko la mtoto kutoka kwa mama huyo. Kulingana na mamake Wangui, bintiye alilazimika kumuuza mwanawe ili kulipia deni la matibabu hospitalini, ingawa haijulikani alivyokuwa na deni la hospitali hiyo.
"Nilifanyiwa upasuaji na mtoto wangu akawekwa kwenye kiangulio. Nilipoondoka hospitali leo, nilitakiwa kurejea na mume wangu. Baada ya hapo, tuliarifiwa kuwa mtoto wetu aliaga dunia. Tulitia saini nyaraka zilizohitajika na mwili wake ukapelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti.
"Jana, mwanamke mmoja alinipigia simu na kuniomba kwenda hospitalini kumchukua mtoto wangu. Nilipomuuliza mtoto alikuwa wa nani, hakunijibu. Alitaka nimweleze pesa nilizotumia kwa kununua taulo ya haja ya watoto," Nanjala alisimulia.
Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KENYA: MWANAMKE AKAMATWA NA POLISI AKIJARIBU KUMUUZA KICHANGA KWA SH. 27,000/-
Reviewed by By News Reporter
on
9/12/2018 12:02:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: