Loading...

MAMBO NI MOTO SIMBA SC, WAANZA KUJENGA UWANJA WAO

Loading...
Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa utaanza rasmi ujezi wa Uwanja wake wa mpira uliopo maeneo ya Bunju jijini Dar es Salaam wiki hii.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema baada ya kusimamisha zoezi hilo kwa muda mrefu, rasmi sasa wanarudi na kasi ili kuhakikisha suala hilo linakamilika.

Manara amesema ndani ya wiki hii watawapeleka wanahabari kwa ajili ya kushuhudia rasmi namna taswira nzima ya Uwanja na ramani itakavyokuwa.

Simba imeamua sasa kuanza harakati za ujenzi wake kufuatia kuingia kwenye mfumo mpya wa mabadiliko ambao utaiendesha klabu hiyo katika nyenzo za kisasa.

Harakati za Uwanja huo zinaanza ili kuhakikisha walau kuelekea mwisho wa msimu wa ligi timu iweze kupata nafasi ya kuanza kuutumia kwa kufanyia mazoezi.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAMBO NI MOTO SIMBA SC, WAANZA KUJENGA UWANJA WAO MAMBO NI MOTO SIMBA SC, WAANZA KUJENGA UWANJA WAO Reviewed by By News Reporter on 9/12/2018 12:22:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.