Loading...

KIONGOZI WA UPINZANI NELSON CHAMISA ATANGAZA KUJIAPISHA URAIS WA ZIMBABWE

Loading...
Siku moja tu baada Emmerson Mnagangwa kuapishwa rasmi kuwa rais, kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa amesema kwamba atajiapisha mwenyewe kama rais wa wananchi.

Kiongozi huyo wa chama cha MDC aliwaambia wafuasi wake kwamba yuko tayari kujiapisha kama rais Jumamosi Septemba 15. 

Chamisa pia alisema kuwa Mnangangwa alikataa kukutana naye ili wajadili masuala kadhaa na alidai kwamba atanyanyasa uongozi wake kwa sababu alimuibia kura.

Chamisa alisema kuwa ataunda wizara yake sambamba na Rais Mnangagwa na atafanya kila awezalo kuhakikisha kwamba ananyanyasa uongozi wake. 

"Nitakapoapishwa, nitachukua mkondo wangu na Mnangangwa achukue wake, tutaona ni nani kiongozi dhabiti," Chamisa alinukuliwa na mtandao wa Daily News. " 

Nilitoa wito kwa Mnangangwa aje tujadili masuala kadhaa ila alikataa, nitahakikisha kwamba natatiza vilivyo uongozi wake na hatakuwa na amani kamwe ikizingatiwa kwamba aliniibia kura," Chamisa aliongezea.
Na Mwanaidi Bakari.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KIONGOZI WA UPINZANI NELSON CHAMISA ATANGAZA KUJIAPISHA URAIS WA ZIMBABWE KIONGOZI WA UPINZANI NELSON CHAMISA ATANGAZA KUJIAPISHA URAIS WA ZIMBABWE Reviewed by By News Reporter on 9/12/2018 12:43:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.