Loading...
STAA wa Juventus, Cristiano Ronaldo ameomba aongezewe ulinzi kutokana na kuwa na wasiwasi na usalama wake nchini Italia.
Pamoja na kuwa Ronaldo hajafunga katika mechi tatu za Serie A akiwa na timu yake mpya ya Juventus bado amekuwa kivutio cha mashabiki.
Mathalani katika mechi tatu za ugenini alizocheza Ronaldo dhidi ya Chievo Verona na Parma zote zilijaza mashabiki wa soka, ambao miaka ya karibuni wamepungua sana kwenye Serie A.
Kwa mujibu wa Gazeti la Corriere di Torino, Ronaldo ameomba aongezewe walinzi kwa ajili yake binafsi na familia yake.
Ronaldo ana wasiwasi kuwa mzuka wa mashabiki unaweza kusababisha akavamiwa katika nyumba yake iliyoko eneo la Gran Madre Park mjini Turin.
Staa huyo ameiomba Juventus kumua-ndalia pia walinzi kwa ajili ya familia yake na wengine kwa ajili yake binafsi na hasa wakati wa mechi.
Juventus ipo vizuri kwenye Serie A, ambapo imeshinda mechi zote tatu.
Na Bakari Juma.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

C.RONALDO AHOFIA USALAMA WAKE NCHINI ITALIA, AOMBA ULINZI ZAIDI KWA FAMILIA YAKE
Reviewed by By News Reporter
on
9/09/2018 11:07:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: