Loading...
Mwenyekiti mtendaji na mmiliki wa kampuni ya Alibaba, Jack Ma amesema anampango wa kustaafu nafasi yake mwakani.
Taarifa zilizotumwa kwa njia ya barua kwa washikadau na wateja wa kampuni hiyo, zilitaarifu kung'atuka kwake na kusababisha mkanganyiko juu ya muda wa kuondoka kwake.
Bw. Ma, ni moja ya mtu tajiri nchini China, atamuachia mikoba Daniel Zhang, kwa sasa ni mkurugenzi mkuu.
Alibaba ni moja ya makampuni yenye thamani kubwa duniani - hisa zake zimeongezeka mara mbili ya thamani yake mwaka jana.
Bw. Zhang atakuwa mwenyekiti mtendaji kuanzia tarehe 10 Septemba 2019, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kampuni hiyo.
Bw. Ma, ambaye alikuwa mwalimu wa Kiingereza, alianzisha Alibaba mwaka 1999 na imeonekana kuwa kampuni kubwa ya mtandao duniani.
Bw. Ma, ambaye kwa sasa anautajiri wa dola $36.6 bilioni (Sh. 93.8 trilioni), ataendelea kuwa mkurugenzi wa bodi ya Alibaba hadi mkutano wa wanahisa wa mwaka 2020. Yeye ni mwanachama wa kudumu wa Ushirikiano wa Alibaba.
Bw. Ma, amedai yeye bado ni mdogo katika dunia, kwahiyo anataka kujifunza vitu vipya.
Alisema: "Kitu kimoja ambacho ninaweza kuwahidi ni kuwa Alibaba haimuhusu Jack Ma pekee, lakini Alibaba itamilikiwa na Jack Ma daima."
Alisema pia Bw. Zhang, ambaye amekuwa na kampuni ya Alibaba kwa takribani miaka 11, ameonyesha "kipaji cha kipekee" tangu alipokuwa mkurugenzi mkuu. Kwahiyo namuamini kukaimu nafasi yangu kwa ustawi wa kampuni ya Alibaba.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

'JACK MA' MMILIKI WA KAMPUNI YA ALIBABA ATANGAZA KUSTAAFU RASMI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
9/10/2018 09:49:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: