Loading...
Saratani ni tatizo kubwa kwa binadamu, lakini pia huathiri aina nyingine nyingi za viumbe duniani. Tembo, hata hivyo, wameonyesha uwezo wa ajabu kuepuka ugonjwa huo na utafiti mpya hatimaye unaweza kuonyesha ni kwa nini: imegundulika jeni za "anti-cancer" alizonazo mnyama huyo katika mwili wake ndio ambazo zinalenga na kuua seli zote zenye vinasaba(DNA) zilizokufa.
Jitihada za utafiti, ambazo ziliongozwa na mwanasayansi katika Chuo Kikuu cha Chicago, Marekani, zimefanikiwa kujibu swali kwanini mnyama mkubwa kama tembo anakuwa na kiwango kidogo cha ukuwaji wa kansa kuliko viumbe wadogo, kama vile binadamu. Waligundua kwamba jeni zao zinafanya kazi ya ziada ili kuzuia saratani katika mihimili yake.
Kwa kupima namna seli hai za tembo huitikia uharibifu ambao unaweza kuzifanya kuwa vimelea vya kansa. Wanasayansi waligundua jambo lisilo la kawaida. Protini inayojulikana kama p53, ambayo inauwezo wa kutambua uvimbe kwa mamalia, inafanya kitu tofauti kwa tembo. Inaamsha jeni iliyodhoofika, au kufa inayoitwa LIF6, ni inapotambua vinasaba (DNA) iliyoharibiwa na inaamuru mauaji ya seli ambazo zinaweza kuleta kansa.
Wakati seli zilizoharibiwa zinayeyushwa nje zinakosa hata nafasi ndogo ya kugeuka kwa uvimbe.
Hii ni habari njema kwa wanyama wakubwa kama Tembo, Kifaru na kiboko, lakini vipi kuhusu binadamu? Hakika, hatuwezi kumuwekea mfumo wa uzuiaji wa kansa kwa kutumia jeni za kipekee kama tuonavyo, lakini kwa kujua mchakato wa kuua vimelea vya kansa unavyofanya kazi katika tembo inaweza kutoa tiba mpya zinazofanya kazi kwa njia sawa.
"Labda tunaweza kutafuta njia za kutengeneza madawa ambayo yanaia tabia ya LIF6, tutaendelea kufanyia kazi zaidi swala hili ili tupate matokeo chanya kwa kuhakikisha tunapambana na ugonjwa huu hatari wa kansa," Mwandishi Mwandamizi wa utafiti huo alisema.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
NAMNA TEMBO ANAVYOJIKINGA NA KANSA, YALETA TUMAINI JIPYA TIBA YA UGONJWA HUO
Reviewed by By News Reporter
on
9/10/2018 11:21:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: