Loading...
Urithi wa urais si jambo geni duniani. Kwa mfano, nchini Amerika kumekuwa na familia mbili ambapo baba na mwanae walikuwa marais.
Rais wa pili na sita walikuwa John Adams na kijana wake John Quincy Adams; rais wa 41 na 43 walikuwa George W.W Bush na mwanawe George W. Bush Snr.
Barani Afrika, urithi huu wa urais sio jambo geni. Marais hawa watano pia baba zao walikuwa marais.
1. UHURU KENYATTA - KENYA
Rais huyu wa nne wa Kenya ni mtoto wa Rais Jomo Kenyatta ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Kenya baada ya taifa kujipatia uhuru.
Uhuru aliwania urais wakati akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mjini Hague, Uholanzi.
Uhuru Kenyatta alichaguliwa rais miaka 34 baada ya babake.
2. IAN KHAMA - BOTSWANA
Ian Khama ni mtoto wa rais wa zamani Seretse Khama; Ian akichaguliwa miaka 27 baada ya babake kuondoka madarakani.
Ian alipata urais 2008 kabla kushinda kiti hicho katika kura za bunge 2009. Rais huyo alitetea wadhifa wake katika kinyang’anyiro kilichozua utata mkubwa 2014 na hatimaye kustaafu mapema 2018.
Babake Sereste Khama alileta mageuzi ya ukombozi katika eneo hilo la kusini mwa Afrika, ikilinganishwa na Ian ambaye inasemekana amesababisha kudorora kwa mahusiano na viongozi wengine wa Afrika.
3. JOSEPH KABILA - KONGO
Rais wa sasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) John Kabila ni mtoto wa Rais Laurent Desire Kabila.
John aliingia mamlakani 2001 siku kumi tu baada ya babake kuuawa, na kisha kuchaguliwa tena 2011. Familia ya Kabila imetawala DRC tangu taifa hilo kujinyakulia uhuru.
4. ALI BONGO ONDIMBA - GABON
Ali Bongo ni mtoto wa Omar Bongo ambaye alikuwa uongozini tangu 1967 hadi kufikia kifo chake 2009.
Rais Ali Bongo alishinda kura ya 2009 katika kinyang’anyiro kikali ambacho matokeo yake yaligubikwa na utata mwingi.
5. FAURE ESSOZIMNA - TOGO
Faure alichukua hatamu za uongozi 2005 kufuatia kifo cha babayake Gnassingbe Eyadema. Familia hiyo imetawala Togo kwa miaka 55 tangu taifa hilo kujinyakulia uhuru.
Faure alitwaa urais baada ya kushindwa uchaguzi kwa njia ya kidemokrasia 2005 licha ya shutuma za viongozi wa kimataifa.
Baadaye, alihifadhi kiti hicho cha urais katika chaguzi za 2009 na 2015 licha ya matokeo yenye utata.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
PICHA ZA VIONGOZI WA AFRIKA WALIORITHI URAIS KUTOKA KWA BABA ZAO
Reviewed by By News Reporter
on
9/10/2018 01:11:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: