Loading...

"TUMECHOSHWA NA WEWE NA WANAJESHI WAKO" - RAIA WA UGANDA WAMSHAMBULIA MUSEVEN

Loading...
Rais wa Uganda Yoweri Museveni alishambuliwa vikali na wananchi kufuatia kifo cha hivi majuzi cha afisa wa zamani wa polisi Muhammad Kirumira.

Kirumira na mkewe walipigwa risasi na watu wasiojulikana Jumamosi Septemba 8.

Rais Museveni alifika katika eneo la tukio kuwahutubia wananchi ila hotuba yake ilikatizwa na baadhi ya vijana waliompigia mayowe wakidai wamechoshwa na uongozi wake.

Taarifa ziliarifu kwamba maafisa wa polisi walijaribu kutuliza umati lakini hawakuweza na kumlazimu rais kuondoka bila kutoa hotuba yake.

" Tumechoshwa na wewe pamoja na wanajeshi wako, tunataka uchukue hatua, watu wanaua kiholela usiku na mchana, utaongoza nani? nchi bila wananchi?," Kijana mmoja alisema kama alivyonukuliwa na gazeti la Daily Monitor la Uganda.

Wananchi wengi wamekuwa wakimlaumu Rais Museveni kwa mauaji ya kiholela hasa kwa wale wanaojaribu kukosoa au kupinga serikali yake.
Na Haika Gabriel.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
"TUMECHOSHWA NA WEWE NA WANAJESHI WAKO" - RAIA WA UGANDA WAMSHAMBULIA MUSEVEN "TUMECHOSHWA NA WEWE NA WANAJESHI WAKO" - RAIA WA UGANDA WAMSHAMBULIA MUSEVEN Reviewed by By News Reporter on 9/10/2018 01:48:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.