Loading...

JACKLINE WOLPER ATANGAZA KUOKOKA, WATU WAMPONDEA MAVAZI YAKE

Loading...
Mwanadada mjasiriamali nchini Jackline Wolper ametangaza kuwa kwa sasa hivi ameokoka na anampenda sana yesu ingawa watu wamekuwa wakimshambulia kuwa kwanini habadilishi mavazi yake kama kweli yeye ameokoka.

Hata hivyo Jack anatetea maamuzi yake ya kuingia kwenye uokovu huku akisema kuwa swala la kuokoka aliangalii wapi unaenda au nini unafanya au nini unavaa kwa sababu swala la uokovu ni vile wewe mwenyewe unakuwa na imani ngapi kwa Mungu.

Jack anatolea mfano na kusema kuwa mashabiki wao wamekuwa wakiwaandama sana watu kama hao kama walivyokuwa wakimuandana Muna kipindi ameokoka kutokana na uwepo wa tatoo nyingi mwilini mwake huku wakisema kuwa Muna sio mlokole kabisa.

Jack anasema kuwa watu wengi hasa vijana wamekuwa wakitamani sana kuokoka lakini wamekuwa wakiangalia jinsi wanavyoandamwa pale wanapoanza kusali huku wakiwa wametangaza kuwa wameokoka na kuona kama itakuwa ngumu kwao kuokoka lakini wapo wengi ambao wanaku wa na mionekano ya kimjinimjini na wanataka kuokoka.

Hata hivyo Jack anawashauri watu wengine kuο koka huku akiomba kuwa na disco la yesu ambalo wale walitoka katika mambo ya kidunia wasikose kuwa wakifurahia uokovu.
Na Fatma Pembe.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
JACKLINE WOLPER ATANGAZA KUOKOKA, WATU WAMPONDEA MAVAZI YAKE JACKLINE WOLPER ATANGAZA KUOKOKA, WATU WAMPONDEA MAVAZI YAKE Reviewed by GEOFREY MASHEL on 9/03/2018 04:22:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.