Loading...

UJENZI WA MELI MPYA AMBAPO JPM LEO AMESHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MIKATABA YAKE, KUTOA AJIRA 250

Loading...
Kaimu meneja wa Kampuni ya Meli (MSCL) Erick Hamis amesema kwamba ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 yenye tani 400 utatoa ajira 250.

Amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa meli hiyo mpya na ukarabati wa meli nyingine za MV Viktoria na Mv Butiama na ujenzi wa Chelezo.

Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula amesema kwamba baada ya meli ya Mv Bukoba kuzama usafiri ulikuwa wa shida.
“Tunatumia fursa hii kukushukuru(Rais Magufuli) kwa jitihada zako na sisi tutakuunga mkono,’’amesema.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula amesema tukio hilo ni dhahiri kwamba Rais ana dhamira kwa anayoyasema.

Alisema kwamba Rais aliposema anajenga reli kutoka Mwanza alikuwa pia amedhamiria na kwamba miundombinu hiyo itasaidia kukuza uchumi wa Kanda ya Ziwa.

“Wapo watu ambao hawataki kuamini kinachofanyika lakini ukweli ndio huo,’’amesema.
Na David Mchomvu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
UJENZI WA MELI MPYA AMBAPO JPM LEO AMESHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MIKATABA YAKE, KUTOA AJIRA 250 UJENZI WA MELI MPYA AMBAPO JPM LEO AMESHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MIKATABA YAKE, KUTOA AJIRA 250 Reviewed by GEOFREY MASHEL on 9/03/2018 05:03:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.