Loading...
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku wananchi kusambaza picha zinazoonyesha mtu anayeugua ugonjwa wa Ebola ambazo zinapotosha jamii.
Amesisitiza kupitia mfumo wa ufuatiliaji kuhusu ugonjwa wa Ebola hadi sasa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini na ufuatiliaji unaendelea.
Ummy ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 3, 2018 wakati wa ufunguzi wa semina ya waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo yenye lengo la kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kuondoa hofu miongoni mwao.
Amesema kuna baadhi ya picha ambazo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikipotosha jamii kuwa zinatokea hapa nchini.
"Zile picha si za Tanzania na kuzisambaza ni kinyume na sheria, na kutokana na hilo tutatoa taarifa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kudhibiti usambazaji huo," amesema Waziri Mwalimu.
Hivi karibuni, Waziri Mwalimu alitangaza kutokea kwa mlipuko wa kumi wa Ebola nchini DR Congo.
Mikoa iliyotajwa kuwa hatarini ni ile iliyoko mipakani ambayo ni Kagera, Katavi, Rukwa na Songwe.
NA Mussa Kitoi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

WAZIRI UMMY APIGA MARUFUKU WANANCHI KUSAMBAZA PICHA POTOFU ZA WAGONJWA WA EBOLA
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
9/03/2018 03:04:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: