Loading...

MWANAMUZIKI BEBE COOL WA UGANDA ADAI BOBI WINE ANATUMIA MAJERAHA YA KUGUSHI KUJIPATIA UMAARUFU

Loading...
Mwanamuziki wa Uganda mwenye utata Bebe Cool amezungumza kwa mara ya kwanza kumhusu Bobi Wine baada ya tamasha yake kukatizwa na watu waliompiga vijembe kwa kukosa kusimama na Bobi katika masaibu yake. 

Bebe alizomewa jukwani huku raia wakiimba ‘Mwachilieni Bobi Wine’ pamoja na kumrushia vifaa tofauti alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki katika tamasha ya ‘Swangz Avenue All-Star’ eneo la Lugogo Cricket Oval jijini Kampala siku ya Ijumaa, Agosti 31.

Akizungumza na kituo cha runinga cha NTV cha nchini Uganda siku moja baada ya kuzomewa jukwani, Bebe alidai kuwa Waganda walikuwa sawa kuwasilisha malalamiko yao lakini kwa mtu ambaye hakustahili kuyapokea.

Nyota huyo wa ‘Tubonga Nawe’ ambaye hakuwahi kuzungumzia masaibu ya Bobi Wine alisema haungi mkono dhuluma alizotendewa mwenzake, lakini akadai kuwa huenda amebuni majeraha ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.

“Wanahabari, NTV, mna kamera, ukimtazama bobi akishuka kwenye gari baada ya vikao vya mahakama, aliegemea gari kwa mkono mmoja na kushika mikongonjo kwa mkono mwingine. Ni nini kilichokuwa hapo? Alikuwa amesimama hewani au kwa kutumia miguu yake? 

“Vyombo vya habari, mnamtazama Bobi aliyevalia viatu vizito zaidi maishani, moja ambayo mgonjwa hawezi kutembea navyo kwa urahisi kwa kuwa ni nzito sana na hamuwezi kuchanganua hilo,” Bebe alieleza.
Na Neema Joshua.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MWANAMUZIKI BEBE COOL WA UGANDA ADAI BOBI WINE ANATUMIA MAJERAHA YA KUGUSHI KUJIPATIA UMAARUFU MWANAMUZIKI BEBE COOL WA UGANDA ADAI BOBI WINE ANATUMIA MAJERAHA YA KUGUSHI KUJIPATIA UMAARUFU Reviewed by GEOFREY MASHEL on 9/03/2018 01:43:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.